Sunday 26 January 2014

Hahaha ! Crazy phone conversation !!

By Tagawah
Bint:: Hallo mpenzi, mambo!
Jamaa:: Poa baby!
Bint:: Uko wapi?
Jamaa: Mimi niko town napata lunch.
Bint:: Wow! Unarudi saa ngapi? Nina
njaa dear, nataka uniletee msosi.
Jamaa:: Narudi baada ya nusu saa,
Nikuletee nini?
Bint:: Niletee chipsi kuku, soseji, mayai
manne yakaangwe pembeni, baga,
piza ya samaki waweke mayonaize,
coka take away ya baridi, mkate wa
moto kwenye ile bekari ya Wapemba
na maji ya kunywa chupa kubwa ya
Kilimanjaro.
Jamaa: Umesahau viti, meza, leseni,
masufuria, sahani na vijiko.
Bint::Kwa nini dear?
Jamaa::Naona hutaki kula,unataka
kufungua hoteli!!

No comments:

Post a Comment